Historia Ya Ukraine - Wikipedia, Kamusi Elezo Huru
Có thể bạn quan tâm
Yaliyomo
hamishia kwenye mwambaa upande ficha- Mwanzo
- Makala
- Majadiliano
- Soma
- Hariri
- Hariri chanzo
- Fungua historia
- Soma
- Hariri
- Hariri chanzo
- Fungua historia
- Viungo viungavyo ukurasa huu
- Mabadiliko husika
- Pakia faili
- Kiungo cha daima
- Maelezo ya ukurasa
- Taja ukurasa huu
- Pata URL iliyofupishwa
- Switch to legacy parser
- Tunga kitabu
- Pakua kama PDF
- Ukurasa wa kuchapika
- Wikimedia Commons
- Wikidata kifungu
Historia ya Ukraini inahusu eneo la Ulaya ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Ukraini (au Ukraina).
Historia ya kale
[hariri | hariri chanzo]
Ukraini ulianza polepole pamoja na Urusi huko makabila ya wasemaji wa Kislavoni cha Mashariki walikoanza kujenga maeneo yao kuanzia karne ya 8 BK.
Waviking waliunda dola la kwanza katika eneo la Kiev, wakalitawala kama dola la Kislavoni. Wenyewe waliingia haraka katika lugha na utamaduni wa wenyeji, lakini waliacha jina lao kwa sababu "Rus" kiasili ilikuwa jina la Waskandinavia wale kutoka Uswidi ya leo.
Mwaka 988 Kiev ilipokea Ukristo wa Kiorthodoksi kutoka Bizanti. Tukio hilo liliathiri moja kwa moja utamaduni na historia yote iliyofuata.
Dola la Kiev liliporomoka kutokana na mashambulio ya Wamongolia baada ya Jingis Khan, na maeneo madogo zaidi yalijitokeza yaliyopaswa kukubali ubwana wa Wamongolia.
Upanuzi wa utemi wa Moscow
[hariri | hariri chanzo]
Katika karne ya 14 sehemu kubwa ya maeneo ya Milki ya Kiev ya awali ilifikishwa chini ya utawala wa Polandi na Lithuania. Tawi moja la familia ya watawala wa Kiev lilidhibiti Moscow katika mashariki-kaskazini. Hapa viongozi wake walifaulu kuimarisha utawala na kupanua eneo lake. Hata askofu mkuu wa Kiev, aliyepaswa kuondoka baada ya kuchomwa kwa mji wake, hatimaye alihamia Moscow. Hivyo watawala wa utemi wa Moscow walijitazama kama wafuasi halali wa Dola la Kiev wakaendelea kutumia jina "Rus" lililoendelea kuwa chumbukizo la jina Urusi. Hatimaye watemi wa Moscow walifaulu kushinda pia Wamongolia na kupata uhuru.
kutoka katikati ya karne ya 15 hadi katikati ya karne ya 18, ardhi ya kati na kaskazini mwa Ukraini ilidhibitiwa na Kossaki ya Kiukraini, kiongozi wao wa kwanza alikuwa Ostafy Dashkevich (mkuu wa jiji la Cherkasy) na wa mwisho alikuwa Petro Kalnyshevskyi.
Maeneo makubwa ya Ukraini ya leo yalikuwa chini ya utawala wa Lithuania na Polandi na baadaye ya Ufalme wa Maungano ya Poland-Lithuania. Mwaka 1696 watawala wa Polandi walishawishi sehemu ya maaskofu Waorthodoksi kukubali maungano na kanisa katoliki na hii ilikuwa chanzo cha kutokea kwa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina.

Kuanzia 1648 hadi 1657, vita vya ukombozi vilipiganwa nchini Ukraini chini ya uongozi wa Bohdan Khmelnytsky dhidi ya Polandi, alijaribu kuunda serikali huru kwa Waukraini, lakini kwa sababu ya usawa wa nguvu, alilazimika kuhitimisha muungano na Moscow. Ukraini ilipokea haki za taasisi inayojitegemea, lakini serikali ya Urusi ilipunguza polepole uhuru huu, hadi mnamo 1775 Kossaki za Kiukraini ziliharibiwa. Hati zao zote za thamani, ambazo ni ushahidi wa historia ya Ukraini katika karne ya 15-18, zilihifadhiwa kwa muda mrefu katika ngome ya St. Elizaveta (leo mji wa Kropyvnytskyi).
Sehemu ya Ukraini upande wa mashariki wa mto Dnestr ilitawaliwa na Moscow. Katika karne ya 18 Polandi iligawanywa kati ya majirani yake. Ugawaji huo uliongeza sehemu za Ukraini zilizofika chini ya utawala wa Urusi. Ila sehemu ya kusini-magharibi ilikuwa sehemu ya milki ya Austria. Katika maeneo chini ya Urusi Wakatoliki walipaswa kurudi katika Kanisa la Kiorthodoksi. Lakini katika maeneo yaliyochukuliwa na Austria tangu mwaka 1772, serikali iliwapa Wakatoliki Waukraini haki sawa na Kanisa la Kilatini; liliweza kuunda seminari na vyuo; taasisi hizo zikawa chimbuko la kukua kwa lugha ya Kiukraini na utaifa wa Kiukraini.
Miaka mia ya mwisho
[hariri | hariri chanzo]Miaka 1918 - 1921, baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na ya kuporomoka kwa Dola la Urusi, nchi ilikuwa na kipindi kifupi cha uhuru na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Miaka 1922 - 1991 Ukraini ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti. Jamhuri hiyo ilikuwa moja ya nchi wanachama walioanzisha Umoja wa Mataifa.[1] Hali halisi haikuwa na madaraka ya pekee kwa sababu ilikuwa chini ya usimamizi wa serikali kuu ya Moscow.
Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti nchi ilijipatia tena uhuru wake kama Jamhuri ya Ukraini, ingawa Russia haikuridhika wala kukubali mipaka.
Mwaka 1991 Urusi na Ukraini ziliutia sahihi mkataba wa urafiki walipoahidiana kuheshimiana kama majirani wema.
Kwa msingi huo, mwaka 1994 Ukraini ilikabidhi Urusi silaha za nyuklia iliyowahi kurithi kutoka jeshi la Kisovyeti na kwenye Mkataba wa Budapest Urusi, Marekani na Uingereza ziliahidi kulinda Ukraini katika mipaka yake dhidi ya mashambulizi yoyote[2].
Hata hivyo, baada ya mwaka 2000 majadiliano ndani ya Ukraini kuhusu kujiunga na umoja wa NATO ilianza kuleta ugumu katika uhusiano na Urusi.
Mwaka 2013 yalitokea maandamano na mapigano kwa sababu rais Viktor Yanukovich aliamua ghafla kukataa mapatano ya kujiunga na Umoja wa Ulaya yaliyokwisha kukubaliwa tayari. Waandamanaji kwa mamia waliuawa na polisi na hatimaye rais alikimbilia Urusi. Hapo bunge liliamua kumwondoa madarakani na kuwa na uchaguzi mpya wa rais.
Katika hali hiyo Urusi ilivamia Krim kwa njia ya kuficha. Wanajeshi wasio na sare walitokea kwenye miji ya Krim wakivamia majengo ya serikali pamoja na bunge la kieneo[3]. Idadi isiyojulikana ya wabunge la jimbo la Krim waliamua tarehe 5 Februari kuondoa serikali ya jimbo wakaitisha kura za wananchi. Tarehe 11 Februari walitangaza uhuru wa Krim, na kura ya wananchi ya tarehe iliyoendeshwa na mamlaka mpya ilitangaza kuwa na kura nyingi za kujiunga na Urusi. Ombi hilo lilikubaliwa na Urusi.
Mnamo Aprili 2014 waandamanaji walivamia majengo ya serikali huko Donetsk wakidai pia kura kuhusu kujitenga na Ukraini. Baada ya kuondolewa na polisi, waandamanaji wenye silaha walitangaza maeneo ya Donetsk na Luhansk kuwa "jamhuri za kujitegemea". Serikali ya Ukraini iliongeza polisi na pia jeshi. Mapigano yalianza ambako jeshi la Urusi lilisaidia waasi, kwanza kwa siri na baadaye waziwazi. Mapigano hayo yalikuwa mwanzo wa Vita ya Donbas iliyoendelea hadi mwaka 2022.
Mwaka 2022 rais wa Urusi alitangaza kwamba yeye haoni Ukraini kama nchi halisi akaamuru jeshi lake kuvamia Ukraini tarehe 24 Februari.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Activities of the Member States - Ukraini". United Nations. Iliwekwa mnamo 2011-01-17.
- ↑ https://treaties.un.org/doc/Publication/UNTS/Volume%203007/Part/volume-3007-I-52241.pdf Memorandum on security assurances in connection with Ukraine’s accession to the Treaty on the Non-Proliferation of Nuclear Weapons, Tovuti ya treaties.un.org, iliangaliwa Machi 2022
- ↑ Gunmen Seize Government Buildings in Crimea, gazeti la New York Times ya 27 Februari 2014
| |
|---|---|
| Nchi huru | Albania· Andorra· Armenia1· Austria· Azerbaijan1· Belarusi· Bosnia na Herzegovina· Bulgaria· Udeni· Estonia· Georgia1· Hispania· Hungaria· Isilandi· Eire· Italia· Kazakhstan2· Kroatia· Kupro1· Latvia· Liechtenstein· Lituanya· Luxemburg· Malta· Masedonia Kaskazini· Moldova· Monako· Montenegro· Norwei· Polandi· Romania· San Marino· Serbia· Slovakia· Slovenia· Ubelgiji· Ucheki· Ufalme wa Muungano· Ufaransa· Ufini· Ugiriki· Uholanzi· Ujerumani· Ukraine· Ureno· Urusi2· Uswidi· Uswisi· Uturuki2 |
| Nchi zisizokubaliwana umma wa kimataifa | Abkhazia1· Kosovo· Kupro ya Kaskazini1· Ossetia ya Kusini1· Transnistria |
| Maeneo yanayojitawalachini ya nchi nyingine | Akrotiri na Dhekelia1· Åland· Azori· Faroe· Gibraltar· Guernsey· Jan Mayen· Jersey· Madeira· Man· Svalbard |
| 1 nchi ya Asia ya Magharibi kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya kiutamaduni 2 nchi ya kimabara | |
| Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Ukraini kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- Mbegu za historia
- Ukraine
- Historia ya Ukraine
- Historia ya Ulaya
Từ khóa » Vita Ya Urusi Na Ukrain Leo
-
Yaliyojiri Leo Katika Vita Vya Urusi Na Ukraine 14.06.2022 - YouTube
-
Yaliyojiri Leo Katika Vita Vya Urusi Na Ukraine - YouTube
-
Yaliyojiri Leo Katika Vita Vya Urusi Na Ukraine 31.05.2022 - YouTube
-
Vita Vya Ukraine: Je Makubaliano Ya Magharibi Kuipinga Urusi ...
-
Urusi Na Ukraine: Ushindi Kwa Ukraine Au Kushindwa Kwa Putin ...
-
Ukraine | Matukio Ya Kisiasa | DW | 07.08.2022
-
Urusi: Habari, Podcasts, Video Na Uchambuzi - RFI
-
Urusi - UN News - The United Nations
-
Vita Ya Urusi Na Ukraine Leo 24032022 - TikTok
-
BBC Swahili - Urusi Yateka Meli Za Kivita Za Ukraine... | Facebook
-
Yaliyojiri Leo Katika Vita Vya Urusi Na Ukraine 29.06.2022 (9.18 MB)
-
Matokeo Ya Vita Baridi Yajirudia Katikati Ya Mkakati Mpya Wa ...
-
Urusi | JamiiForums
-
Urusi: Vituo Vya Kijeshi Vya Ukraine Vyashambuliwa Kwa Makombora