JamiiForums
Có thể bạn quan tâm
JamiiForums URUSI: Zaidi ya Watu 724 kutoka Miji 32 wanashikiliwa na Vyombo vya Usalama kwa kupinga mpango wa Kuandikishwa kupigana Vita #Ukraine#Russia imeidhinisha kifungo cha hadi Miaka 10 kwa Mwanajeshi yeyote atakayejisalimisha, kujaribu kuacha Jeshi au kukataa kupiganaZaidi - https://jamii.app/VitaniUkraine#RussiaUkraineWar 👍9😢2 3.32K viewsedited 08:25 JamiiForums MAREKANI KUINGILIA KATI URUSI IKITUMIA NYUKLIAKauli hiyo imetolewa baada ya Rais wa Urusi, #VladimirPutin kutoa vitisho hivyo katika vita dhidi ya #UkraineMarekani haijafafanua ni kwa namna gani itajibu mapigo moja kwa mojaSoma - https://jamii.app/PutinNuclear#RussiaUkraineWar 👍17🔥3😁3 3.38K views03:19 JamiiForums UFARANSA: Mamilioni ya raia wameandamana wakiishinikiza Ufaransa kujitoa NATO na Rais Emmanuel Macron kujiuzulu Pia, wameitaka Serikali kuacha kutoa silaha kwa #Ukraine kutokana na Uhaba wa Mafuta uliosababishwa na Vikwazo dhidi ya #Russia Soma https://jamii.app/ParisProtests#Democracy 👍20😁5👎2 3.14K views10:53 JamiiForums Maofisa kadhaa wa Marekani wamesema Kombora lililoua Watu wawili #Poland, lilirushwa na Ukraine wakati wa kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka kwa vikosi vya Urusi#Ukraine bado ina miliki silaha zilizotengenezwa na UrusiSoma https://jamii.app/PolandUkraine#PolandMissileStrike 👍9 3.18K viewsedited 10:54 JamiiForums UNESCO: WAANDISHI 86 WALIUAWA MWAKA 2022Mauaji ya Waandishi na Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari yameongezeka kutoka vifo 55 kwa Mwaka 2021Vifo vingi vilitokea #Mexico (19), #Ukraine (10) na #Haiti (9). Mwaka 2018 (99), 2019 (58) na 2020 (62)Soma https://jamii.app/KuuawaWaandishi#PressFreedom 👍2👎2 2.48K views11:58 JamiiForums MWILI WA NEMES TARIMO KUSAFIRISHWA JANUARI 24, 2023Mwili wa Mtanzania huyo anayedaiwa alifariki akiwa vitani #Ukraine utasafirishwa kutoka #Russia kuelekea #Tanzania kwa ajili ya mazishiFamilia imesema Ubalozi bado haujawajulisha muda wa kuwasiliSoma https://jamii.app/MwiliWaNemes 👍1 2.28K views14:08 JamiiForums URUSI: HATARINI KUFUNGWA MIAKA 10 JELA KWA KUPOSTI KUHUSU VITA INSTAGRAMOlesya Krivtsova (20) yupo chini ya uangalizi akituhumiwa kwa Ugaidi baada ya kuweka Maudhui katika ukurasa wake akiikosoa #Russia kuhusu vita dhidi ya #UkraineSoma https://jamii.app/RussiaDigital#DigitalRights 👍4 2.41K views05:18 JamiiForums #DIPLOMASIA: Marekani imeanza mashauriano na Washirika wake wakiwemo Kundi la Nchi 7 Tajiri Duniani (G7) ili kuiwekea vikwazo China> Ni baada ya kuituhumu #China kuwa inataka kuisaidia #Urusi Silaha za kupambana na #UkraineSoma https://jamii.app/USSanctions#Governance 👎9👍1 2.37K views05:38 JamiiForums Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa Hati ya kumkamata Rais #VladimirPutin kwa maelezo kuwa amehusika na Uhalifu wa Kivita kufuatia uvamizi wa #UkraineWizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema "Maamuzi ya #ICC hayana maana kwasababu Nchi hiyo haipo kwenye Mkataba wa #Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, hivyo haiwajibiki chini yake"Una maoni gani kuhusu hatua hii ya ICC dhidi ya Rais Putin?Soma https://jamii.app/PutinICC#Accountability #HumanRights 😁15👍10👎3🤡2 2.66K views17:08 JamiiForums VIONGOZI 6 WA AFRIKA KUSULUHISHA MGOGORO WA URUSI NA UKRAINERais wa Urusi, #VladimirPutin na Rais wa #Ukraine, #VolodymyrZelenskyy wote wamekubali kupokea ujumbe huo kutoka Afrika Kusini, #Senegal, Misri, #DRCongo, #Uganda na #ZambiaSehemu ya masharti ya mazungumzo, Ukraine inataka Urusi iondoe Majeshi yake katika ardhi yake wakati Urusi inashinikiza Ukraine ikubali kuliachia eneo la #CrimeaSoma https://jamii.app/RussiaUkraineAfrica#RussiaUkraineWar #Governance 👍6 2.2K views05:02 JamiiForums AFRIKA KUSINI KUBADILI SHERIA ILI KUKWEPA KUMKAMATA PUTINUamuzi huo unatarajiwa kufanyika ili Taifa kuwa na nguvu ya kuamua mtu wa kumkamata pindi anapotuhumiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (#ICC)Hoja hiyo imeibuka baada ya Rais wa Urusi, #VladimirPutin kuwa na mwaliko wa kushiriki katika kikao Agosti 2023 Nchini Afrika Kusini na yupo hatarini kukamatwa kutokana na Vita inayoendelea baina ya Urusi na #Ukraine lakini wenyeji wake hawataki akamatwe kwa kuwa wao hawana upande katika vita hiyo Chama cha Upinzani cha Democratic Alliance (#DA) kimesema kitafungua kesi kupinga uamuzi wa Serikali kwa kuwa wao wanataka Putin akitua Afrika Kusini akamatweSoma https://jamii.app/SouthAfricaICC#Diplomacy #Governance 👍4❤1 2K views06:09 JamiiForums #RUSSIA: Kiongozi Mkuu wa Jeshi Binafsi la Wagner, #YevgenyPrigozhin, amesema hawakuwa na lengo la kumpindua Rais #VladimirPutin na Serikali yake bali walitaka kuzuia uharibifu dhidi ya Jeshi hiloMmiliki huyo wa #WagnerGroup amesema "Lengo letu lilikuwa kuonesha masikitiko na kuwawajibisha Maafisa ambao kwa vitendo vyao visivyo vya kitaalamu wamefanya makosa mengi."June 24, 2023 kulikuwa na ripoti kuhusu Kundi la Wagner linalosaidiana na #Urusi katika Vita ya #Ukraine kutofautiana na Serikali ya Putin hali iliyoibua hisia za mapinduzi Nchini humoSoma https://jamii.app/WagnerVsPutin#JamiiForums #HumanRights #JFMatukio #Diplomacy #Governance 😁6👍5 2.54K views18:35 JamiiForums Kitendo cha Viongozi wa #NATO kudai #Ukraine inapaswa kujiunga na Muungano wa Kijeshi wa Umoja huo siku zijazo pindi masharti yatakapotimizwa bila kuyataja wala kutaja muda, kimemfanya Rais #VolodymyrZelenskyy kukosoa mchakato huo dhidi ya Taifa lakeKupitia #Twitter, Rais Zelenskyy amekosoa uamuzi huo kwa kuandika "Ni jambo lisilo la kawaida na la kipuuzi kutoweka muda wa mwaliko au uanachama wa #Ukraine."Soma https://jamii.app/ZelenskyyNATO#Diplomacy #Governance #RussiaUkraineWar #JamiiForums 👍10 1.96K views08:36 JamiiForums URUSI: Mwanaharakati #AlexeyNavalny ambaye amekuwa akipinga waziwazi Utawala Rais #VladimirPutin, alikuwa akituhumiwa kuunda na kufadhili Genge lenye itikadi kali, pia kuendesha Uasi dhidi ya Serikali Hukumu hiyo iliyosomwa ndani ya Magereza ambapo Navalny anatumikia Kifungo kingine cha Miaka 11 kwa kuhamasisha Maandamano ya kupinga uamuzi wa #Russia kuivamia #Ukraine, imepingwa na Umoja wa Ulaya (EU) wakieleza inadhihirisha Ukandamizaji wa #Haki na #UhuruWaKujieleza nchini humoSoma https://jamii.app/PutinRival#JamiiForums #Governance #HumanRights #FreeSpeech #FreedomOfExpression 👍6 2.4K viewsedited 12:24 JamiiForums MASON MOUNT APATA MAJERAHA, KUIKOSA MECHI DHIDI YA ARSENALKiungo wa #ManchesterUnited, #MasonMount anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mmoja baada ya kuumia katika mchezo uliopita ambao timu yake ilifungwa magoli 2-0 dhidi ya #TottenhamHotspurMount aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 60 (Tsh. Bilioni 191) atakosa mechi mbili za #PremierLeague dhidi ya #NottinghamForest (Agosti 26) na #Arsenal (Septemba 3), pia atakosa michezo ya timu ya Taifa ya #England dhidi ya #Ukraine na #Scotland (Septemba 9 na 12)Soma https://jamii.app/MountUpdates#JFSports #JamiiForums 👍3❤1 2.29K views03:56 JamiiForums URUSI: #MarinaOvsyannikova Mwandishi wa Habari aliyeshiriki maandamano wakati wa Matangazo Mubashara 'Live' kwenye Televisheni akipinga uvamizi wa Urusi dhidi ya #Ukraine, amehukumiwa kwenda Jela miaka 8.5 bila yeye kuwepo MahakamaniKwa mujibu wa Mahakama, Ovsyannikova (44) anayeishi uhamishoni Paris, Ufaransa amekutwa na hatia ya "Kusambaza hadharani habari za uongo licha ya kuwa na ufahamu kuhusu matumizi ya Vikosi vya Wanajeshi wa Urusi"Ovsyannikova amesema "Ni hukumu isiyo na Haki, Urusi hakuna haki Mahakamani, Rais ameharibu mfumo, hata ushahidi waliotoa juu yangu ni wa uongo."Soma https://jamii.app/Ovsyannikova#Democracy #RussiaUkraineWar #FreedomOfSpeech #FreePress #Justice #JamiiForums 👍8👎1 2.42K views05:16 JamiiForums UTAFITI: Mwaka 2023 umetajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi ya Raia ndani ya kipindi cha Miaka 10 iliyopita kulingana na Utafiti wa Shirika la Kutoa Misaada Kuhusu Vurugu za Kivita (AOAV) la EnglandOngezeko la vifo kwa Asilimia 112 ni kutoka Mwaka 2022 hadi 2023 ambapo vita ya #Israel na #Hamas imechangia kwa kiasi kikubwa ikifuatiwa na migogoro inayoendelea Urusi na #Ukraine, Sudan, #Myanmar na #SomaliaMilipuko ya 2023 ilikuwa 7,307 kutoka 4,322 ya Mwaka 2022, vifo vya Raia vilikuwa 15,305 na matumizi ya silaha zinazorushwa hewani yaliongezeka kwa 226% (kutoka matukio 519 hadi 1,694)Soma https://jamii.app/Milipuko2023#HumanRights #CivilRights #Governance #JamiiForums 👍4❤1 3.43K views04:31 JamiiForums MAREKANI: Mauzo ya Silaha za kwenda nje ya nchi kwa Mwaka 2023 yameongezeka kwa 56% na kufikia Dola Bilioni 238 (Tsh. Trilioni 604) kulinganisha na mwaka 2022 huku vita ya Urusi dhidi ya #Ukraine ikizidisha mahitaji hayoPoland ambayo ipo katika harakati za kupanua Jeshi lake, nayo ni kati ya Mataifa yaliyonunua Silaha nyingi zikiwemo Helikopta za Apache kwa Dola Bilioni 12 (Tsh. Trilioni 30), Mfumo wa Roketi (Himars) Dola Bilioni 10 (Tsh. Trilioni 25), Dola Bilioni 3.75 (Tsh. Trilioni 9) kwa Vifaru vya M1A1 Abrams na Mfumo wa Ulinzi wa Anga Dola Bilioni 4 (Tsh. Trilioni 10)Wakati huo huo, Utawala wa Rais #JoeBiden umesema kitendo cha kuiuzia silaha Ukraine, kinasaidia kukuza uchumi wa ndani wa MarekaniSoma https://jamii.app/UasWeapons#Diplomacy #Governance #JamiiForums 👍9❤1 2.8K viewsedited 05:26 JamiiForums #URUSI: Kiongozi wa upinzani, #AlexeiNavalny, ametangazwa kufariki akiwa Gerezani. Navalny alikuwa mkosoaji mkubwa wa Rais #VladimirPutin, na alikuwa akitumikia kifungo cha Miaka 19 kwa makosa yanayodaiwa kuwa ya KisiasaAlihukumiwa kwa kuhamasisha Maandamano ya kupinga uamuzi wa #Russia kuivamia #Ukraine, kuunda na kufadhili Genge lenye itikadi kali, pia kuendesha Uasi dhidi ya Serikali.Soma https://jamii.app/AlexeiNavanlyDies#JamiiForums #Governance #HumanRights #FreeSpeech #FreedomOfExpression #Democracy 👍3 2.77K views13:09 JamiiForums URUSI: Rais #VladimirPutin amesaini amri inayoruhusu kukamatwa kwa mali za Raia wa Marekani na Kampuni zao zilizopo Urusi ikiwa ni sehemu ya fidia ya Vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya #MoscowAmri hiyo ya Putin itazipa Kampuni za Urusi, Mashirika na Watu binafsi walioathiriwa na vikwazo, haki ya kuomba fidia kwa Serikali ya Urusi kisha Serikali itatumia mali za Marekani kuwalipaNchi za Magharibi zilizuia mali za Urusi zenye thamani ya Dola Bilioni 300 (Tsh. Trilioni 776), baada ya Moscow kupeleka Wanajeshi kuivamia #Ukraine Februari 2022Bunge la Marekani lilipitisha Sheria ya REPO inayoruhusu Utawala wa Rais #JoeBiden kuchukua mali za Urusi zinazoshikiliwa katika Benki za Marekani ili kuisaidia UkraineSoma https://jamii.app/PutinConsificateUS#JamiiForums #Governance #Diplomacy 👍14❤3🤔1 2.48K views05:51
Từ khóa » Vita Urusi Na Ukraine Jamii Forum
-
Urusi | JamiiForums
-
Ukraine | JamiiForums
-
가입 - Facebook
-
Tunachofahamu Kuhusu Vifo Vya Wanajeshi Wa Urusi Nchini Ukraine ...
-
Je, Mzozo Huo Unagharimu Uchumi Wa Urusi Kwa Kiasi Gani? - BBC
-
Jamii Forums On Twitter: "Rais Wa Urusi, Vladimir Putin Anatarajiwa ...
-
Urusi Na Uturuki Zajadili Usafirishaji Wa Nafaka Za Ukraine - DW
-
Facebook - Workplace
-
Siku Ya Ushindi Putin Awapongeza Wanajeshi Wake Kwa Kuitetea ...
-
Đại Diện Ukraine Tại Việt Nam Trải Lòng Về Chiến Sự Nga-Ukraine - PLO
-
BREAKING,HALI INATISHA HOFU YATANDA,VITA YA URUSI NA ...
-
Ukraine Xác Nhận Vòng đàm Phán Trực Tuyến Mới Với Nga | Châu Âu
-
Tin Tức Tình Hình Chiến Sự Nga Tấn Công Ukraine Mới Nhất Hôm Nay